Maalim Seif Shariff Hamad akiwapongeza na kuwashukuru wana jumuiya ya Waislamu wa Washingon DC ( TAMCO ) na kuwataka waendelee na umoja walionao na mshikamano kwani huo ndio utamaduni wetu na muongozo wa dini.
Maalim ahudhuria futari iliyoandaliwa na Tanzania Muslim Community Marekani
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amewashukuru na kuipongeza Tanzania Muslim Community kwa juhudi zake za kufutarisha kila wiki ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Maalim alihudhuria iftar siku ya Jumamosi, Juni 11, 2016 jijini Washington DC wakati akiwa katika ziara yake ya siku 14 nchini Marekani na Canada.
Mheshimiwa Ismail Jussa Mkurugenzi wa wa mambo ya nje wa CUF mmoja wajumbe ulioambata na Maalim Seif Shariff Hamad akisalimia na kutoa shukran wa Wanajumuiya ya Waislamu ya Washington DC.