Wednesday, June 29, 2016

Makamo wa Rais Mstaafu wa Zanzibar akutana na Waislamu wa Washington DC


 Maalim Seif Shariff Hamad akiwapongeza na kuwashukuru wana jumuiya  ya Waislamu  wa Washingon DC ( TAMCO ) na kuwataka waendelee na umoja walionao na mshikamano kwani huo ndio utamaduni wetu na muongozo wa dini.
Maalim ahudhuria futari iliyoandaliwa na Tanzania Muslim Community Marekani
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amewashukuru na kuipongeza Tanzania Muslim Community kwa juhudi zake za kufutarisha kila wiki ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani. Maalim alihudhuria iftar siku ya Jumamosi, Juni 11, 2016 jijini Washington DC wakati akiwa katika ziara yake ya siku 14 nchini Marekani na Canada.


Mheshimiwa  Ismail Jussa Mkurugenzi wa wa mambo ya nje wa CUF  mmoja wajumbe ulioambata na Maalim Seif Shariff Hamad akisalimia na kutoa shukran wa Wanajumuiya ya Waislamu ya Washington DC.



Mwenyekiti wa jumuiya ya  Kiislam  ya watanzania inayounganisha majimbo matatu  Washington DC, Maryland, naVirginia (DMV) Sheikh Ali Mohammed, akitoa neno kwa waumini waliohudhuria, mbele ya mgeni rasmi Maalim Seif Shariff Hamad

Blog is under construction

Blog  Waislamu wa Marekani is under construction.